ISLAMABAD,PAKISTAN

WATU wasiopungua kumi wakiwemo magaidi wanne wameuawa katika shambulio dhidi ya soko la hisa la Pakistan, lililoko katika mji wa bandari wa Karachi. 

Kamanda wa polisi wa kanda Sharjeel Kharal,aliviambia vyombo vya habari kwamba walinzi wanne wa usalama,Ofisa mmoja wa polisi na raia mmoja ni miongoni mwa waliouawa. 

Aliongeza kwamba magaidi wote wanne waliuawa, na kwamba watu wengine saba, wakiwemo askari polisi watatu walijeruhiwa katika shambulio hilo. 

Mkurungenzi Mtendaji wa soko la Hisa la Pakistan Farrukh Khan, alisema shambulio hilo lilikuwa zito, lakini kwa bahati nzuri magaidi hawakuweza kuingia eneo kuu la jengo la soko hilo.

Zaidi ya wafanyabiashara na wafanyakazi 1,000 walikwepo katika jengo wakati wa shambulio kwa mujibu wa ripoti.