LONDON, England

MCHEZAJI mpya wa Chelsea Timo Werner ameahidi kuiunga mkono Leipzig katika ligi ya mabingwa  na kusema kuwa anaweza kutua mjini Lisbon kuhudhuria mechi hiyo ya robo fainali.

Werner alikuwa roho ya timu ya Leipzig’s kwenye mafanikio yake ya kombe la  Europe msimu huu, akipachika mabao manne na kutoa usaidizi wa mabao mawili, lakini mshambuliaji huyo miaka 24 hatakuwa sehemu ya wachezaji wa kikosi hicho mwezi Agosti.

Mkataba wa mshambuliaji huyo na Chelsea unaanza Julai 1, ambao unamfanya asiweze kucheza mashindano yajayo huko Ureno.

Chelsea inayonolewa na  Frank Lampard ililala kwa mabao 3-0 nyumbani mbele ya Bayern Munich katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora, na kubaki katika matumaini madogo ya kusonga mbele.

‘’Lakini mimi ni mchezaji wa Chelsea kuanzia Julai 1 na ninalipwa na Chelsea, ‘Werner aliiambia Sportbuzzer’’