LONDON, England

TIMU za Manchester United, Chelsea, Arsenal na Manchester City zitakutana kwenye nusu fainali ya kombe la FA.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na FA timu Manchester United itakutana na Chelsea na Manchester City itakuwa uso kwa uso na Arsenal.

United ilifikia hatua hiyo kwa kuifunga Norwich,  na United imeshinda kombe hilo mara 12,wakati Chelsea iliyoitoa Leicester imeshinda kombe hilo mara nane na Arsenal imetwaa ubingwa huo mara 13 .

Mechi zote hizo zitachezwa kwenye dimba la Wembley wiki ya Julai 18 na 19. Na fainali kupigwa Jumamosi ya Agosti 1 uwanja huo huo.

Ratiba ya michezo hiyo ilipangwa wakati wa mchezo wa Manchester City na Newcastle, na Pep Guardiola alishinda 2-0 shukrani kwa mabao ya Kevin de Bruyne kwa penalti na Raheem Sterling.

Nusu fainali ya baina ya United na Chelsea inakumbusha nusu fainali ya mwaka 2018,ambapo Chelsea ilishinda  .