MILAN, Itali

BAADA ya kumalizana na klabu ya Bologna Julai 18 kwa kuishushia kichapo cha mabao 5-1 sasa AC Milan ina kibarua cha kumenyana na Sassuolo leo Julai 21.

Mchezo huo wa Seria A, AC Milan walitawala kwenye idara ya ushambuliaji ambapo mpaka dakika 90 zinakamilika walipiga jumla ya mashuti 20 yaliyolenga lango huku wapinzani wao wakipiga mashuti manane pekee.

Mabao yalipachikwa na Alexis Saelemaekers dakika ya 10, Hakan Calhanoglu dakika ya 24, Ismael Bennacer dakika ya 49, Ante Rebic dakika ya 57 na bao la mwisho lilipachikwa na Davide Calabria dakika ya 90+2.

Bao pekee la upinzani lilifungwa na Takehiro Tomiyasu dakika ya 44 na kuwafanya wapoteze mazima pointi tatu kwenye mchezo huo.

Ushindi huo umeifanya AC Milan kufikisha jumla ya pointi 56 ikiwa nafasi ya saba huku Bolgna ikiwa nafasi ya 10 na pointi 43 na kinara ni Juventus mwenye pointi 77.