CAIRO, Misri
SHIRIKISHO la Soka la Afrika (Caf), limeahirisha fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), zilizotarajiwa kufanyika mwaka ujao 2021 hadi Januari 2022, kutokana na mripuko wa ‘corona’.


Lakini mashindano kama hayo upande wa wanawake imefutwa.
Katika habari nyingine, kinyang’anyiro cha kombe hilo miongoni mwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika (CHAN) ambayo yangelichezwa mwezi Aprili sasa yatafanyika Januari 2021.

Michuano yote miwili inatarajiwa kufanyika nchini Cameroun.
“Afya ndio kitu muhimu kwetu lazima tuwe macho”, rais wa Caf, Ahmad Ahmad, alisema katika mkutano na vyombo vya habari akitangaza uamuzi huo.
Hatua hiyo ina maana ya kwamba michuano hiyo inayofanyika mara mbili kwa mwaka sasa itafanyika mwaka mmoja na Kombe la Dunia 2022, kitu kilichofanyika mara ya mwisho mwaka 2010.

Michuano hiyo ilifanyika mwaka 2013 huku mashindano ya mwaka huo yakifanyika mwaka mmoja baada ya mwaka huo ili kuzuia kuwa katika mwaka mmoja na Kombe la Dunia, uamuzi ambao ulihatarisha kuyapatia fursa Mataifa ya Afrika katika Kombe la Dunia kwa kuyaongezea msimu wa mashindano.


Huku michuano hiyo ikitarajiwa kufanyika Januari kama ilivyo kawaida, mashindano ya hivi karibuni ya AFCON 2019 yalihamishwa na kufanyika katika msimu wa joto katika juhudi za kuzuia kuingiliana na mashindano ya ligi za Ulaya.


Hatua hii pia ilitarajiwa kuathiri kombe hilo nchini Cameroun, lakini, ikabadilishwa hadi Januari kutokana na hali ya hewa nchini humo mbali na uwezekano wa kuingiliana na michuano ya Kombe la Dunia.


Uamuzi huo unamaanisha kwamba mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Liverpool watacheza msimu wote ujao bila ya kuwapoteza washambuliaji wao hatari, Sadio Mane na Mohamed Salah katika mechi za kimataifa.

Wakati huohuo kufutiliwa mbali kwa kombe la michuano ya mataifa bingwa ya Afrika miongoni mwa wanawake kumeshangaza wengi wakati ambapo kinyanganyiro hicho kilikuwa hakina muandalizi.


Hata hivyo, mashindano ya wanawake yalipigwa jeki kutokana na uzinduzi mpya wa Kombe la Mabingwa Afrika 2021 miongoni mwa wanawake. (BBC Sports).