WANADAMU daima wameathiri kwa njia moja au nyengine masuala yao ya mazingira, kutoka moto hadi kilimo.
Lakini ushawishi wa binadamu Duniani umefikia kiwango ambacho sasa unashawishi matukio yaliopo.
Kutoka kwa uchafuzi wa hewa kwenye anga za juu hadi vipande vya plastiki chini ya bahari, haiwezekani kupata mahali duniani ambapo binadamu hajapaathiri kwa njia yoyote.
Lakini kuna wingu jeusi katika upeo wa macho yetu.
Zaidi ya asilimia 99 ya viumbe ambavyo vimeishi duniani vimeangamia, vingi wakati wa majanga kama yale yaliouawa madubwana.
Binadamu hawajawahi kukabiliwa na tukio la kiwango kama hicho, lakini hivi karibuni ama baadaye huenda wakaathiriwa.
”Mwisho wa mwanadamu hauepukiki”
Kwa wataalam wengi swali sio kwamba binadamu wataangamia lakini iwapo binadamu watawahi kuangamia, na hiyo itakuwa lini.
Na kuna wengine ambao wanafikiria huenda ikawa karibuni na sio baadaye.
Mwaka 2020, mtaalamu wa masuala ya virusi Frank Fenner alisema kwamba huenda tukaangamia karne ijayo, kutokana na idadi kubwa ya watu, uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya hali ya anga.
Maisha yataendelea na makovu tutakayowacha duniani yatapotea kwa haraka sana.
”Miji yetu itaangamia, misitu itamea na madaraja yataanguka. Na baadaye asili yetu itaozesha kila kitu”, anasema Alan Weisman, mwandishi wa kitabu cha The World without us, kilichochapishwa 2007 na ambacho kinaangazia ni nini kitakachofanyika iwapo binadamu atatoweka duniani.

Iwapo hawezi kuvivunja atavizika. Na muda mfupi baadaye, kila kitu kilichowachwa na binadamu kitabadilika na kuwa plastiki.
Ushahidi wa haya yote ni kutazama eneo la dunia ambalo tumelazimishwa kuishi.
Katika eneo la maili 19 linalozunguka kiwanda cha umeme cha Chernobyl nchini Ukraine, ambacho kilichafuliwa kufuatia kulipuka kwa kinu cha kinyuklia, mimea na wanyama sasa wanaishi katika eneo hilo vizuri zaidi ya ilivyokuwa.
Utafiti uliofadhiliwa na baraza la utafiti kuhusu mazingira uligundua idadi kubwa ya wanyamapori katika eneo hilo, ikimaanisha kwamba binadamu sio hatari kwa mazingira yaliopo ikilinganishwa na miaka 30 ya mionzi mikali.
Kasi ambayo asili husimamia mazingira ya eneo fulani inategemea na hali ya anga.
Katika eneo la jangwa la mashariki ya kati uharibifu uliofanywa maelfu ya miaka iliopita unaonekana, lakini sio kwa miji ya miaka mia moja iliopita katika msitu wa tropiki.
Mwaka 1542, wakati wazungu walipoona misitu ya mvua nchini Brazil, waligundua miji, barabara, mashamba kandakando ya mito mikubwa.
Hatahivyo, baada ya wakaazi kuangamia kutokana na magonjwa yalioletwa na wageni hao miji hiyo ilichukuliwa na wanyama.
Ni wazi kwamba uharibifu wa Las Vegas utaendelea kwa kipindi kirefu ukilinganishwa na ule wa mji wa Bombay.
Ni wakati huu ambapo ukataji miti na mbinu za kuhisi mbali zinaweza kutupatia kile kilichokuwa kikifanyika hapo awali.
Mimea na wanyama ambao wamekuwa na uhusiano wa karibu na binadamu ndio watakaoathirika pakubwa iwapo wanadamu wataangamia.
Mimea inayotumiwa na wanadamu kama chakula ambayo hutegemea dawa za kuuwa wadudu na mbolea itaangamia na badala yake mimea mingine kuchipuka.
”Mimea hiyo itarithiwa kwa haraka”, anasema Wiseman. Karoti zitabadilika na kuwa mwitu.”
Kutoweka mara moja kwa dawa za kuuwa vidudu kutasababisha ongezeko la wadudu.
Wadudu hutembea, huzaana haraka na kuishi katika mazingira yoyote, na hivyobasi kuwafanya kuonekana kama wanyama wanaoweza kufanikiwa kwa haraka licha ya kwamba binadamu wanajaribu kuwapunguza.
”Magonjwa ya biblia” ambayo uharibu mimea yatakuwa hatari zaidi utokana na mabadiliko ya anga.
”Yanaweza kuongezeka na kuzoea kwa haraka zaidi ya kitu chochote kile duniani, isipokuwa pengine viini”, anaelezea Weisman.
Kitu chochote kinachofanana na mlo kitaliwa.
Ongezeko la wadudu badala yake litaongeza idadi ya wanyama wanaowala kama vile, vindege, panya, mjusi na popo huku nao pia wakiongeza idadi ya wanyama wanaowala.
Lakini kila kinachopaa jua lazima kishuke. Idadi kubwa haitaendelea kuishi katika kipindi cha muda mrefu wakati chakula kilichowachwa na wanadamu kitatoweka.
Kuangamia kwa wanadamu kutakuwa na athari katika mtandao wa chakula kwa takriban miaka 100, kabla ya hali mpya ya kawaida kuanza kuonekana.
Baadhi ya ng’ombe mwitu pamoja na kondoo wataendelea kuishi, lakini wengi wao walifugwa kama wanyama wanaokula polepole na wakaidi hatua itakayowafanya kuangamia kwao kwa idadi kubwa.
”Nadhani punde tu wataliwa na wanyama pori”, alisema Weisman.
”Wataliwa na wanyama kama paka zaidi ya mbwa. Nadhani mbwa mwitu watafanikiwa pakubwa na watashindana na mbwa wa kawaida”, alisema Weisman.
Paka hufanikiwa pakubwa kila wendapo.Swali la iwapo maisha ya kiintelijensia yataendelea tena ni gumu kujibu.
Nadharia moja kwamba intelijensia itaendelea ni kwasababu iliwasaidia mababu zetu kuweza kukabili athari za kimazingira.
Mabadiliko yanayoweza kuwaathiri nyani katika maeneo yao wanayoishi yanaweza kutokea kutokana na matatizo ya kuangamia kwa binadamu.
Lakini iwapo sote tutaangamia kesho, itachukua maelfu ya miaka kwa gesi ya kijani iliojaa angani kurudi kama ilivyokuwa kabla ya kuanza kwa viwanda.
Hali ya anga inabadilika kwa kasi kuu na katika mwelekoo hatari sana: imesema ripoti ya wanasayansi inayoonya kuhusu takwimu za viwango vya joto duniani.
Halafu kuna tatizo la vinu vya kinyuklia. Ushahidi wa kinu cha nyuklia cha Chernobyl unaonesha kwamba mazingira yanaweza kujiponya kutokana na mionzi.
Lakini kuna takriban vinu 450 vya kinyuklia duniani ambavyo vitaanza kuyeyuka punde tu mafuta ya majenereta ya vinu hivyo yatakapokwisha.
Hakuna njia ya kubaini athari za kuvuja kwa mionzi katika mazingira. Na hilo ni kabla hatujaanza kufikiria kuhusu uchafuzi mwengine wa mazingira.

Miongo inayokuja baada ya kuangamia kwa binadamu itaathriwa na umwagikaji wa mafuta, kuvuja kwa kemikali na milipuko ya viwango vya aina yake ya mabomu yote ambayo mwanadamu atakuwa ameyawacha.
Baadhi ya matukio hayo yanaweza kusababisha mioto ambayo inaweza kuwaka kwa miono mingi.
Chini ya mji wa Centralia katika jimbo la Pennsylvania, safu ya mkaa imekuwa ikiwaka tangu 1962, na hivyobasi kulazimu wenyeji wa enoo hilo kuondoka na mji huo kuharibiwa.
Hii leo eneo hilo linaonesha barabara zilizotengenezwa mbali na moshi unaofuka. Asili imechukua sakafu ya eneo hilo.
Hatahivyo athari za mwanadamu zitasalia hata makumi ya mamilioni ya miaka baada ya kuangamia kwake.
Viini vitakula plastiki ambazo zitawachwa na mwanadamu. Barabara na magofu yatasalia kwa maelfu ya miaka lakini hatimaye yatazikwa ama hata kuharibiwa na nguvu za asili.