Nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara zinaongoza kwa umasikini

IKIWA dunia iko katika kukabiliana na umasikini, bado dunia inaonesha kukabiliwa na umasikini mkubwa ambapo katika kisichozidi kizazi kimoja, zaidi ya watu bilioni 1.1 ‘wamekwamuliwa kutokana na umaskini’, kwa mujibu wa Benki ya Dunia.

Hakuna shaka hii ni habari nzuri kuhusu ustawi wa dunia katika karne hii.

Kati ya 1990 na 2015, idadi ya watu duniani wanaoishi kwa chini ya dola 1.90 – kiwango cha umaskini wa kimataifa – kilishuka kutoka watu bilioni 1.9 hadi watu milioni 735.

Hii inamaanisha sehemu ya idadi ya watu wanaotazamwa kuwa maskini, kwa ufafanuzi huo, imeshuka kutoka asilimia 36 hadi asilimia 10 katika kipindi hicho.

Lakini suala la vita dhidi ya umasikini haliko sawa na mwanauchumi aliyeweka kiwango hicho cha umasikini aliiambia BBC kuwa sera za hivi sasa za maendeleo “haziwafikii masikini kisawasawa”.

Martin Ravallion, aliyekuwa mkurugenzi wa utafiti na kaimu mkuu rais wa Benki ya Dunia amesema kuwa “Changamoto kubwa katika siku zijazo ni kuongezeka kwa ukosefu wa usawa inayoathiri maendeleo dhidi ya umaskini na mandeleo mapana zaidi ya kijamii”.

Kwa mujibu wa benki ya Dunia, ukuwaji wa kutoshirikishwa, kudorora kwa uchumi na kwa hivi karibuni zaidi, mizozo, zimeathiri maendeleo au hatua kupigwa katika baadhi ya mataifa.

Wakati nchini China na India idadi jumla ya watu bilioni moja sio masikini tena, idadi ya watu walio masikini sana Afrika, kusini mwa jangwa la sahara ipo juu kuliko ilivyoshuhudiwa miaka 25 iliyopita.

“Katika muongo mmoja uliopita, tumeona dunia ikisogea kwa kasi mbili,” anasema Carolina Sánchez-Páramo, mkurugenzi wa kimataifa wa mpango wa Poverty and Equity Global Practice katika benki ya Dunia.

Sababu ya hili ni mchanganyiko wa masuala manne, ameiambia BBC.

1. Kasi tofuati za ukuaji wa uchumi

“Katika kiwango cha msingi, ukuaji umepungua katika mataifa ya Afrika kusini mwa jangwa la Sahara na Amerika ya kusini kuliko Asia mashariki na kusini katika muda huu na ukilichanganya hilo na idadi inayokuwa ya watu katika mataifa mengi, inayotokana na kuongezeka kiwango cha watoto wanaozaliwa, unachopata ni kiwango kilicho chini mno dhidi ya ukuwaji,” anasema.

“Wakati mataifa hayakui, ni vigumu kupiga hatua katika kukabiliana kupunguza umaskini, kwasababu hatua yoyote itatokana na usambazaji upya na mkubwa na hilo ni vigumu kulifanya.”

2. Ukuaji unaojumuisha pande zote

Lakini wakati ukuaji wa uchumi endelevu ni “sharti muhimu” katika kupunguza umaskini, sio “suala la pekee”, mkurugenzi huyo wa Benki ya Dunia anasema.

Katika mataifa mengi ukuwaji “haujajumuisha pande zote kwa kiasi cha kutosha”, kutokana na hali ya viwanda ambavyo vinaajiri watu wachache mfano katika Afrika ya kusini mwa jangwa la Sahara.

Bi Sánchez-Páramo amesema: “Ajira ndio chanzo kikuu cha kipato kwa walio masikini. hivyo kama hakuna nafasi za kutosha za ajira, huenda ikawa vigumu kuona umasikini ukipungua.”

3. Kufikia miundo msingi

Uchumi huimarika wakati sio tu watu wana kipato cha pesa lakini pia wakati wanapata elimu, ufadhili na miundo msingi mizuri.

Iwapo hayo hayapatikani, Bi Sánchez-Páramo anasema, “Hilo pia linashusha hadhi kiwango cha ukuwaji unaojumuisha pande zote”.

Nchini Malaysia, kwa mfano, na kusini na mashariki mwa Asia, “angalau baadhi ya mambo haya yanasogea kwa wakati sawa,” anaongeza.

Kwa viwango vya kimataifa, umaskini Malaysia umekuwa katika kiwango cha sifuri tangu 2013 – lakini sio kwa kiwango cha nchi hiyo.

4. Mizozo

Hatimaye, katika miaka ya hivi karibuni, mizozo ya kisiasa na vita imefutilia mbali hatua zilizopigwa katika siku za nyuma kwenye baadhi ya mataifa.

“Wakati huo huo, umaskini ni kuangazia mataifa yalio dhaifu na yalioathirika na mizozo, kwasababu baadhi ya matiafa mengine yamefanikiwa kupiga hatua,” anasema Bi Sánchez-Páramo.

Mnamo 2015, Nusu ya idadi ya watu maskini wapo katika mataifa matano – India, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Ethiopia na Bangladesh.

Na utabiri wa hivi karibuni unaashiria kuwa Nigeria imeipiku au inakaribia kuipiku India kua taifa lenye idadi kubwa ya watu wanaoishi katika umaskini – mataifa yote yakiwa na karibu watu milioni 100 masikini.

Kufikia 2030, licha ya uchumi wa mataifa mengiya Afrika kupiga hatua katika vita dhidi ya umaskini, karibu watu 9 kati ya 10 wanaishi kwa doola 1.90 kwa siku au kiwango cha chini zaidi kusini mwa jangwa la Sahara.

Kuwafikia walio masikini zaidi

Kuangamiza umasikini kufikia 2030 ni mojawapo ya malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa mataifa, lakini ripoti yake mnamo Julai imesema makadirio yanaonyesha asilimia 6 ya idadi jumla ya watu duniani watakuwa wanaishi chini ya kiwango cha umaskini kimataifa kufikia tarehe hiyo ya mwisho.

Makadirio ya benki ya Dunia yana unafuu kidogo katika kumaliza viwango vya umaskini kuwa chini ya asilimia 3 ya idadi jumla ya watu, lakin ikwa hali ilivyo huenda kiwango hicho kisifikiwe duniani.

Bwana Ravallion anasema sera zilizopo za maendeleo “zinawafaa watu walio masikini lakini sio kwa watu walio maskini sana”.

Lakini anaamini kwamba “walio maskini sana hawafikiwa ipasavyo”.

“Ukirudi siku za nyuma na unapofikiria ulimwengu wa sasa tajiri, miaka 200 iliyopita watu walikuwa maskini kama ilivyo Afrika leo.”

“Walivyokwepa umaskini ni kwa kuwafikia walio maskini zaidi taratibu lakini kwa ufanisi zaidi. Hilo ni kinyume cha ulimwengu unaoendelea leo.”

Mataifa tajiri yalifanikisha uwezo na sera kutimiza utoaji huduma kwa jamii nzima, kama vile elimu na afya.

“Hapo ndipo ulimwengu wa sasa unaoendelea unapojivuta nyuma. Unafanikiwa kupunguza kwa kasi idadi ya maskini lakini haufanikiwa kuwafikia walio maskini zaidi,” anasema Ravallion.