MILAN, Itali

BEKI wa klabu ya Lazio Patric amepigwa marufuku ya mechi moja baada ya kumuuma mchezaji wa Lecce wakati wa mchezo wa ligi ya Italia Serie.

Mlinzi huyo alipoteza mwelekeo na kuamua kumng’ata Giulio Donati wakati wa mchezo wao wa ligi uliochezwa Jumanne Julai 7.

 Patric alitakiwa kutoka nje ya uwanja baada ya kitendo chake cha dakika ya mwisho wa mchezo baada ya timu yake inayokaribia kushuka daraja kumaliza mchezo ikiwa imefungwa magoli mawili kwa moja.