KIGALI,RWANDA
BIASHARA zinazomilikiwa na wanawake zimeongezeka kwa zaidi ya asilimia 40 katika mfumo wa ikolojia wa Kigali, na kuongeza kiwango cha wastani cha kimataifa kwa mujibu wa utafiti mpya.
Watu 403 waliohojiwa katika uchunguzi wa Ekolojia ya Ujasiriamali ya Kigali, asilimia 41 walikuwa na mwanzilishi mwanamke .
Wajasiriamali wanaojishughulisha na ICT na kilimo wana idadi kubwa ya mipango ya msaada, tofauti na utalii.
Zaidi ya asilimia 75 zilikosa ufadhili wa nje, hali ambayo iinayopelekea changamoto katika mfumo wa uanzishaji wa ikolojia wa Kigali.
Akizungumzia utafiti huo, Aneth Batamuliza, mjasiriamali na kiongozi wa utafiti alisisitiza hitaji la juhudi za jamii kukuza mazingira ya biashara ya Kigali.
“Mfumo wetu wa mazingira unazunguka kila wakati na wachezaji wapya, wafanyabiashara na mashirika yanayounga mkono ikolojia,” alisema.
“Ili kuleta mazingira ya ujasiriamali kuwa mbali zaidi, lazima sote tushirikiane, tutambue mapungufu na kushinikiza kwa ufanisi mfumo bora wa mazingira ambao tungetaka kujenga”,alisema.