NEWYORK, Marekani
MWANARIADHA Usain Bolt amemtambulisha binti yake na jina lake wakati wa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mama wa mtoto wake.
Mtoto huyo ametajwa kuwa ni Olympia Bolt. Kwenye ujumbe wake Bolt amesema anamtakia mama wa mtoto mchanga.
Kasi Bennett, siku nzuri ya kuzaliwa yenye furaha, akiahidi kuwa atafanya bidii ili mama huyo na binti yake waendelee kutabasamu kila siku.
Mashabiki wa Bolt wamekuwa wakisubiri kwa hamu kuona sura ya mtoto huyo na kujua jina lake.