NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

BUNDI ananyemelea kutua kwenye benchi la ufundi la kikosi cha Yanga kwa kile kinacho zungumzwa kwamba kocha mkuu wa kikosi hicho hamuhitaji Boniface Mkwasa.

Yanga jana wameshuka dimbani mkoani Morogoro kuvaana na Mtibwa Sugar bila uwepo wa kocha wao msiadizi.

Ili kuthibitisha habari hiyo Gazeti la Zanzibar Leo, lilimtafuta kocha mkuu wa klabu hiyo Luc ili kupta ukweli wa jambo hilo, ambapo alikiri kuwa kocha msaidizi hajasafiri na timu lakini hawezi kueleza lolote juu ya suala hilo.

“Nikweli kocha msaidizi hajasafiri lakini sina jambo lolote nitakalosema juu ya hilo,”alisema

Huku Kaimu Katibu Mkuu wa  Yanga  Simon Patrick alipotafutwa kuzungumzia sakata hilo alisema watatoa taarifa rasmi Jumatatu.