WASHINGTON,MAREKANI

JIMBO  la California limefuta mipango yake ya kulegeza masharti yaliyowekwa ya kukabiliana na virusi vya corona.

Hatua hiyo ilijiri kufuatia ongezeko la idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya corona katika jimbo hilo na majimbo kadhaa nchini Marekani.

Gavana wa California Gavin Nesom aliamuru migahawa yote pamoja na mabaa na kumbi za filamu kufungwa tena.

Katika jimbo hilo tajiri zaidi na lenye idadi kubwa zaidi ya watu Marekani, makanisa, maeneo ya mazoezi pamoja na maduka makubwa, ambayo huduma zao si muhimu pia yalitakiwa kusitisha shughuli zao za ndani katika nusu ya jimbo hilo ambalo limeathiriwa zaidi.

Jimbo la California lilikuwa la kwanza kutangaza amri ya kusalia majumbani.

Mnamo mwezi Mei liliruhusu biashara kadhaa kufunguliwa, lakini sasa ongezeko la idadi ya maambukizi limelilazimisha kurejesha tena vizuizi.