NA WAANDISHI WETU

WAJUMBE wa mkutano mkuu wadi, masheha na mabalozi katika majimbo jana wamewachagua viongozi katika ngazi ya udiwani katika zoezi la uchaguzi linaloendelea ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kuwapata wagombea wake.

Akifungua mkutano wa uchaguzi wa nafasi ya udiwani katika wadi Jang’ombe Urusi, mwenyekiti wa CCM wadi hiyo, Khamis Usi aliwataka wajumbe kuhakikisha wanachagua viongozi bora.

Alihimiza kwa wapiga kura hao kuweka mbele maslahi ya CCM badala ya kuangalia ubinafsi na kuwasisitiza wachague viongozi watakao saidia kukipatia ushindi chama hicho.

Katika uchaguzi huo Abdulatif Omar Haji alishinda nafasi ya udiwani wadi ya Urusi kwa kupata kura 35 akifatiwa na Burhani Ali aliepata kura 26, ambapo katika wadi ya Kwalinatu Ahmada Ame Ahmeid alishinda kwa kupata kura 54.

Kwa upande wa wadi ya Migombani, Jacob Josef alishinda nafasi ya udiwani o baada ya kupata kura 19 kati ya 67 ambapo kura moja iliharibika akifatiwa na Adinani Ali aliepata kura 13.

Mkoa wa Kaskazini ‘B’

Wadi ya Mkataleni aliyeshinda ni Omar Haruna kwa kura 72 kati ya 144 zilizopigwa na wajumbe na kumtangaza Mzee Othman Abdi kushika nafasi ya pili kwa kupata kura 54

Wadi ya Vijibweni Abuu Haji na Omar Khamis alishinda kwa kupata kura 59, ambapo katika wadi Fujoni aliyeshinda ni Mwajuma Yussuf.

JIMBO LA DIMANI

Katika wadi ya Chukwani, Fatma Rashid Juma alishinda kwa kupata kura 47 akifuatiwa na Hassan Mdachi Hassan aliepata kura 19 na Rahma Mzee Kheir aliepata kura 11.

JIMBO MAHONDA

WADI Mbaleni Hassan Amour ameongoza kwa kupata kura 75, ambapo katika wadi ya Kiwengwa aliyeshinda ni Omar Ramadhan kwa kupata kura 31.

JIMBO LA KIKWAJUNI

Wadi ya Kisimamajongoo aliyeshinda ni Ibrahim Khamis Fatak kwa kura 43 na katika wadi ya Rahaleo aliyeshinda ni Mbarouk Abdalla Said kwa kupata kura 44.

JIMBO LA MALINDI

Wadi ya Mlandege aliyeshinda ni Kinunu Rashid Slim kwa kura 65 na kwa  upande wa wadi ya Malindi aliyeshinda Ali Juma Ali aliepata kura 18.

JIMBO LA PANGAWE

Wadi ya Kijitoupele aliyeshinda Saleh Yahya Saleh kwa kupata kura 73 na katika wadi ya Pangawe aliyeshinda ni Amour Mwita kwa kura 47.

JIMBO LA MWERA

Wadi ya Mwera wajumbe wa mkutano walimchagua Ali Mussa Hassan aliepata kura 52 ambapo katika wadi ya  Kianga alieshika nafasi ya kwanza ni Hamduni Hemed Rashid kwa kupata kura 40.

JIMBO LA AMANI

Wadi ya Amani aliyeshinda Makame Khamis Ame aliepata kura 70 na katika wadi ya Kilmahewa nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Akida Juma Makame aliepata kura 23.

JIMBO LA MAGOMENI

Wadi ya Magomeni alishika nafasi ya kwanza ni Ali Haji Haji ‘China’ kwa kura 69 na katika wadi ya Sogea nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Mohammed Said Mohammed ‘Bonge’, kwa kura 105.

JIMBO LA CHUMBUNI

Wadi ya Mwembemakumbi nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Haji Juma Faki kwa kura 66, wadi ya Chumbuni alieshika nafasi ya kwanza ni Ambari Ujudi Bamba kwa kura 50.

Habari hii imetaarishwa na MWAJUMA JUMA, HAFSA GOLO NA KHAMISUU ABDALLAH