MWANDISHI WETU

CHAMA cha siasa ni maungano ya watu wanaotafuta mamlaka katika dola na hasa serikali kwa kusudi la kutekeleza shabaha za kisiasa au za kifalsafa pamoja na faida kwa ajili ya vikundi fulani faida zao za binafsi.

Vyama mara nyingi hutamka mwelekeo au itikadi fulani inayoandikwa katika programu yao.

Katika mfumo wa vyama vingi kila chama kinagombea nafasi za bunge au serikali dhidi ya vyama vingine.

Wakati wa uchaguzi kila chama kinapaswa kujieleza, kutetea matendo yake ya nyuma na kuonyesha jinsi kinavyotaka kuboresha mambo tofauti na vyama vingine.

Kwa njia hii kila chama huchangia harakati ya kujenga nia ya jamii inamofanya kazi kama inashinda au kushindwa kwenye uchaguzi.

Kwa mukhtaza huo basi dhana hiyo ambayo imekuwa ni vigumu kusimamiwa na viongozi wengi wa kisiasa katika nchi mbali mbali kwa kujali maslahi binafsi.

Pamoja na malengo mazuri ya kuanzishwa vyama vingi vya siasa lakini wako baadhi wamekuwa wakivitumia kwa maslahi yao, jambo ambalo linakwenda hata kinyume na dhana za usajili wa vyama.

Kwa mantiki hiyo basi baadhi ya watu wanadiriki kusema siasa ni mchezo mchafu au njia ya mkato katika kuwapatia mahitaji yao ya fedha na mambo mengine kama hayo.

Hakika uwepo wa vyama vingi vya siasa hapaTanzania hasa visiwa vya Unguja na Pemba ambapo kihistoria vimeonesha kubobea kisiasa kufuatia mbinu, mikakati, busara na maamuzi mazito yaliofanyika mwaka 1964 na kuleta uhuru na heshima ya Wazanzibar.

Kitendo hicho kingekuwa darasa tosha kwa wanasiasa na wafuasi wao ambacho kimefunza jinsi gani wananchi wanastahiki kutumia fursa za kijamii na maendeleo ya kiuchumi yaliomo nchini mwao

Hata hivyo, lakusikitisha hivi sasa baadhi ya wanasiasa wanatumia karata ya vyama vingi kuleta utashi, ubinafsi na kuzalisha chuki zisizo na msingi wala maslahi kwa taifa badala ya kushindana kwa hoja na kubainisha dhamira zao za kushindana kimaendeleo.