KAMPALA,UGANDA

UGANDA  imesema mafanikio iliyopata katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa SDG, yameathiriwa na mripuko wa maambukizi ya COVID-19.

Waziri wa mambo ya ujumla ya nchi hiyo kwenye ofisi ya waziri mkuu Mary Karooro Okurut, alisema ingawa mripuko huo umekuwa na athari kwenye njia ya nchi hiyo ya kutimiza malengo ya maendeleo enedelevu, lakini hautoharibu ahadi ya Uganda ya kutimiza malengo ya ajenda ya mwaka 2030.

Mwakilishi mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Uganda Rosa Malango alisema Uganda inashirikiana na Umoja wa Mataifa kuharakisha kutimiza malengo ya maendeleo endelevu.