NA ARAFA MOHAMED
MKUU wa Wilaya ya Mjini, Marina Joil Thomas, amesema watahakikisha wanafanya jitihada ya kuwasaidia waendesha boti za kutembeza watalii, katika meneo ya Forodhani, na Malindi, katika suala la ulinzi na usalama ndani ya bahari.
Aliyasema hayo, mara baada ya kumalizika kwa ziara ya uwangalizi wa maboti kwa watembeza watalii huko forodha mchanga na Malindi.
Alifahamisha kuwa ni vyema Serikali ya Wilaya hiyo ikafanya jitihada ya kuhakikisha inawapatia vyombo vya ulinzi na usalama, wakati yanapotokea matatizo ili waweze kusaidiana na kuongeza watalii zaidi nchini. Hata hivyo, amewataka waendesha boti hao kuwa na kauli nzuri kwa watalii na kuutunza utamaduni wa kizanzibari hasa katika suala la mavazi kwa watalii hao.
Nao baadhi ya waendesha maboti hayo walisema kutopewa elimu ya kutosha juu ya suala la uwokozi kwa watalii, ikiwemo zimamoto na uwokozi inapelekea kutokea baadhi ya madhara na kusababisha kuwa na uwoga wa kuendesha maboti hayo.
Aidha wamesema kuwa kutopewa elimu ya kutosha juu ya suala la uwokozi kwa watalii hao ikiwemo suala la zima moto inapelekea kutokea baadhi ya madhara na kusababisha kuwa na uwoga wa kuendesha maboti hayo.
Wakizungumza baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya Mjini walisema, ni vyema kwa vyombo vyote viwe na vifaa vya uwokozi ili kuondokana na vifo visivyokuwa vya lazima.