LONDON, England

BEKI wa zamani wa klabu ya Chelsea, Ashley Cole aliyekipiga ndani ya klabu hiyo msimu wa 2006/14 amesema  kipa namba moja wa Manchester United, David de Gea amekuwa kwenye mwendelezo wa makosa awapo langoni jambo lililosababisha timu yake kupoteza kwa kufungwa mabao 3-1 mbele ya Chelsea.

Manchester United, usiku wa kuamkia jana imekubali kupoteza nafasi ya kutinga hatua ya fainali ya Kombe la FA, ambapo iwapo ingeshinda ingekutana na Arsenal iliyokata tiketi ya kutinga fainali baada ya kushinda mabao 2-0 mbele ya Manchester City.

Olivier Giroud wa Chelea alianza kucheka na nyavu  dakika ya 45 akafuatiwa na Mason Mount dakika ya  46 huku nahodha wa Manchester United Harry Maguire akijifunga bao dakika  74 kwenye harakati za kuokoa hatari na lile la Manchester United likifungwa kwa mkwaju wa penalti na Bruno Fernandes dakika ya 89.

Fainali inatarajiwa kuchezwa Agosti 1, Uwanja wa Wembeley ambapo itawakutanisha Arsenal inayonolewa na kocha Mkuu, Frank Lampard na Chelsea inayonolewa na kocha Mkuu, Mikel Arteta.

“De Gea amekuwa akifanya makosa ambayo yanafanana mara nyingi ila anaaminiwa na kocha mkuu, Ole Gunnar Solskjae,r ila hakuwa na chaguo kwa kuwa ni maamuzi yake ni wakati wake wa kufanyia marekebisho makosa yake pamoja na safu ya ulinzi,” amesema.