FATUMA KITIMA, DAR ES SALAAM

SERIKALI imesema kuwa  Uzalishaji wa viwanda unategemea  teknolojia kwa kiasi kikubwa hivyo hakuna budi kuzalisha teknolojia nchini, ili kupata faida kuliko teknolojia kuitoa nje ya nchi.

Akizungumza Jana Dar es Salaam kwenye viwanja vya maonyesho ya 44 ya biashara ya kimataifa sabasaba,  Katibu  Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dokta  Leonard   Akwilapo, amesema hayo, kwenye mjadala wa  Siku ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ambapo imekutanisha Wabuni, Watafiti na Sekta Binafsi .

Dokta Akwilapo alisema tenkonojia ikizalishwa nje ya nchi itakua ghali na inawezekana isiendane na mazingira yake kuliko ikizalishwa nchini.

“Viwanda vikiimarika vikichukua mazao kwa wakulima, watapata faida, Wafanyabiashara pamoja na Viwanda na pato la taifa litaongezeka zaidi”alisema