NA MWANDISHI WETU
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbali mbali za Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Abdulhamid Yahya Mzee walioteuliwa ni Bihindi Nassor Khatib kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Maji na Nishati (ZURA).
Wengine ni pamoja na Asha Ali Abdulla kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA).
Siajabu Suleiman Pandu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na Juma Nyasa Juma ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.
Uteuzi huo wa Rais umeanza rasmi jana julai 22 mwaka 2020.