NA ABOUD MAHMOUD
WAZIRI wa ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Dk. Sira Ubwa Mamboya amewateua wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Karakana Kuu ya Serikali Zanzibar.
Chini ya kifungu cha 7(1) cha tangazo la sheria, wajumbe aliowateua ni Mariam Mliwa Jecha, Hasim Kombo Haji, Ali Kassim Ali, SA. Asia Mohammed Ahmed.
Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Huduma za Matrekta na Zana za Kilimo, Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Karakana Kuu ya Serikali Zanzibar.
Mwenyekiti wa bodi Muhsin Muhammad Ali ambaye tayari ameshateuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi tangu Juni 19 mwaka huu.
Wakati huo huo waziri huyo kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 14(1) cha sheria nambari 10 ya mwaka huu amewateua wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri Barabarani.
Wajumbe walioteuliwa ni Khamis Mussa Khamis, Salim Mohammed Salim, Kamanda wa Polisi Usalama wa Barabarani, Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Barabara Zanzibar, Mkurugenzi Tawala za Mikoa na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri Barabarani.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mtoro Almas Ali ambae uteuzi wake umeteuliwa za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Juni 19 mwaka huu.
Pia kwa uwezo aliopewa waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji chini ya kifungu cha 7(1) cha sheria nambari 11 ya mwaka 2019, amewateua wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara Zanzibar.