KINSHASA,DRC

RAIS Felix Tshisekedi ametangaza kuwa hali ya dharua ya afya dhidi ya janga la COVID-19 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC imeondolewa kuanzia jana.

Rais Tshisekedi pia alitangaza hatua kadhaa za kuchukuliwa katika sekta tofauti nchini.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, wakati wakifuata hatua zilizopo za afya, shughuli za biashara, zikiwemo kufungua mabenki, migahawa na baa, pamoja na mikutano pia zimeanza jana.

Kwa upande wa viwanja vya mpira, kumbi za maonesho, nyumba za ibada, bandari, viwanja vya ndege na mipaka vilipangwa kufunguliwa kuanzia Agosti 15 nchi nzima, wakati watu kutoka mkoa mmoja kwenda mwengine pia wataruhusiwa kuanzia Agosti 15.

Hata hivyo shughuli za mazishi bado zinapigwa marufuku.DRC ina jumla ya watu 8,533 wenye virusi vya corona, huku ikiwa na vifo 196 na waliopona  ni 4,528.