ADDIS ABABA, ETHIOPIA
WAZIRI Mkuu wa Ethiopia ameutaja ujenzi wa Bwawa la An Nahdhah kuwa ni hatua iliyochelewa na kuzionya Misri na Sudan juu ya hatua zao kuhusiana na bwawa hilo.
Abiy Ahmed aliwapongeza wananchi wa Ethiopia kufuatia kumalizika hatua ya kwanza ya kulijaza bwawa lililoibua mzozo la An Nahdhah na kusisitiza kuwa,Mara ya kwanza ya kulijaza bwawa hilo ilimalizika bila ya kumdhuru yoyote.
Waziri Mkuu wa Ethiopia aliongeza kuwa bwawa hilo lilipasa kujengwa kwa uchache miaka 200 iliyopita.
Nchi tatu za Kiafrika ambazo ni Misri, Sudan na Ethiopia zinahitiliafiana kuhusu haki ya kila nchi kwa Mto Nile na namna ya kugawana maji ya mto huo.
Hata hivyo juhudi mbalimbali za kutatua hitilafu za nchi hizo tatu ziligonga mwamba hadi sasa.
Ethiopia ilianza kujenga Bwawa la An Nahdhah mwanzoni mwa mwaka 2011 hata hivyo hitilafu kali baina yake na Misri na Sudan zimepelekea kuakhirishwa mchakato wa ujenzi na kutumiwa maji ya mto huo.