PARIS,UFARANSA

UMOJA wa Ulaya umeliambia shirika la habari la dpa kuwa viongozi wa Umoja huo wamekubaliana kuhusiana na mkakati wa kuhusisha malipo ya fedha za Umoja na sheria.

Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya siku kadhaa za majadiliano bila mapumziko mjini Brussels na wanachama wote 27 wa umoja huo.

Hali hiyo ina maana kwamba umoja wa Ulaya unakaribia makubaliano kuhusiana na fedha za kuunusuru uchumi wa Umoja huo baada ya kukamilika kwa janga la virusi vya corona na pia kupanga bajeti yake kwa miaka ijayo.

Hatua ya kuhusisha fedha za Umoja wa Ulaya na sheria za umoja huo iliwasilishwa na Waziri Mkuu wa Latvia Krisjanis Karins.

Yote hayo yalikubaliwa na nchi zote za Umoja wa Ulaya,viongozi hao lakini bado hawajakubaliana kuhusiana na fedha za muda mrefu za kufufua chumi za nchi zake.