DOHA, Qatar
JUMLA ya mechi nne zitachezwa kila siku katika hatua ya makundi wakati wa fainali zijazo za Kombe la Dunia nchini Qatar zitakazofanyika kuanzia Novemba hadi Disemba 2022.
Haya ni kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ambalo limesema mechi zote za makundi zitapigwa katika kipindi cha siku 12.
Aidha, hakuna ratiba itakayotolewa kuonyesha kwamba mechi fulani zitachezewa katika viwanja fulani mahsusi hadi wakati droo ya mwisho ya fainali hizo itakapotolewa Machi 2022.
Mechi zote za raundi mbili za kwanza zitachezwa kila siku kuanzia saa 7 mchana, saa 10 alasiri, saa 1 jioni na saa nne usiku katika viwanja vinane tofauti.