NA SHAIBU KIFAYA
WAZIRI wa Afya, Hamad Rashid Mohammed, ameutaka uongozi wa
wizara hiyo Pemba pamoja na kitengo cha kichocho na maradhi yasiopewa
kipauombele kusimamia miradi inayoendeshwa kwa fedha za wafadhili nchini.
Kauli hiyo alitoa ofisi ya kitengo cha kichocho
Mkoroshoni Chake Chake, wakati akizungumza na watendaji hao kujua maendeleo ya
mradi wa kutokomeza kichocho na minyoo.
Alisema miradi yote iliyoletwa na wafadhili ni ya serikali, na lengo kuu ni kujitegemea wenyewe kadrii siku zinavyokwenda.
Aidha aliwahimiza wafanyakazi hao kuongeza kasi
ya kufanya kazi kwani kutokana na maelezo ya Mkuu wa kitengo yanaonesha hali ya
ugonjwa huo bado ipo juu.
“Niseme hapo awali tulikuwa tuko vizuri kwa kupungua
ugonjwa huo, lakini ugonjwa wa kichocho bado upo sasa tuzidisheni bidii,”
alisema.