LONDON, England
NAHODHA wa Liverpool, Jordan Henderson, ameshinda tuzo ya mwaka upande wa wanaume ya waandishi wa habari za soka England ( FWA).
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30, aliyeiongoza Liverpool kwenye taji lao la kwanza la ligi katika miaka 30 msimu huu, alipata zaidi ya robo ya kura.
“Nashukuru kama vile sivyo ninahisi kama naweza kukubali hili peke yangu”, alisema.
“Nina deni kubwa kwa watu wengi, lakini, hakuna zaidi ya wachezaji wenzangu wa sasa, ambao wamekuwa vizuri na wanastahili hili kila kidogo kama mimi.”
Wachezaji wenzake wa Liverpool, Virgil van Dijk na Sadio Mane, Kevin de Bruyne wa Manchester City na Marcus Rashford wa Manchester Unite pia walimaliza katika tano bora.
Siku ya Jumatano, Henderson ambaye amepona kutoka kwenye maumivu ya kifundo cha mguu, alipokea taji la Ligi Kuu ya England kutoka kwa mkongwe wa wekundu hao, Sir Kenny Dalglish katika uwanja wa Anfield.
Henderson aliongeza: “Naikubali [tuzo] kwa niaba ya kikosi hichi chote, kwa sababu bila y wao sikuwa katika nafasi ya kupokea heshima hii. Vijana hawa wamenifanya kuwa mchezaji bora, kiongozi bora na mtu bora.
“Kama kuna kitu, natumai walionipigia kura walifanya hivyo kwa kutambua mchango wa timu nzima.”
Henderson pia aliinua taji la Kombe la Dunia la Klabu la Fifa kwa mara ya kwanza mnamo Disemba.
Mshambuliaji wa Arsenal na Uholanzi, Vivianne Miedema, alitajwa bora kwa upande wa wanawake mapema mwezi huu. (BBC Sports).