KILA sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu na rehma na amani zimfikie Mtume wa Mwenyezi Mungu. Ama baada ya utangulizi huu mfupi.

Kwa hakika uislamu ni dini ya amani, upendo na uadilifu, kwani uislamu ni dini pekee ambayo huwalea wafuasi wake juu ya amani, ninakusudia kusema amani ni endelevu na hupelekea watu kufanya mambo yao kwa utulivu kabisa.

Katika makala haya tunazungumzia ibada ya hijja ambayo waislamu huitekeleza kila mwaka huko nchini Saudi Arabia.

Kwa yakini uislamu umechagua nchi yenye Baraka huko Makka na kuitangaza kuwa ni kiwanja chenye amani kwa maana ya ardhi iliyotolewa maudhui na ubabe hapo hukaa muislamu kwa ajili ya ibada ya Mwenyezi Mungu tuu kwa kila utukufu wake na utakatifu wake na amesema kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu. (hivi hawaoni sisi tumeufanya mji huu kiwanja cha amani na watu wanaporwa humo pembezeno.)

Na amani na utukufu wa uislamu katika viwanja hivi vya amani ni kutokana na mauaji na uadui na maudhi na muonekano wowote wa ubabe na akawapa amani watu katika nchi hii juu ya roho zao na mali zoa na heshima zao.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu (Hija ni miezi maalumu basi yeyote atakayehirimia hija basi asifanye maasi wala uchafu wala mijadala kwenye Hija).

Na pia akawapa amani katika viwanja vya Makka hadi ndege na wanyama na hadi wadudu kwa hali yoyote atakapokuwa na udhalili wake isipokuwa wanyama watano ambao huuliwa ndani na nje ya Makka, basi haifai kwa yeyote kukikera chochote katika hivyo kwa ubaya katika eneo la amani kwa kukusudia au makusudi na likifanyika katika hilo kwa lolote kwa makosa ni wajibu kuliunga hilo.

Kwa kila kitu mfano wake katika wanyama au kwa kima chake, kama hakupatikana mnyama kama huyo kama iliyoelekezwa katika sheria ya kiislamu iwe ni kafara ya kitendo hicho kwa kanuni ya kiislamu kwa ujumla na hasa katika viwanja vya Makka tukufu yenye amani bali hadi majani na mimea haifai kuing’oa au kuikata.

Hadithi kutoka kwa Ibni Abbas (RA) kwamba Mtume (SAW) amesema; (Kwa hakika mji huu amekataza  Mwenyezi Mungu , tangu siku alipoiumba mbingu na ardhi nao ni haramu.

Mwenyezi Mungu hadi siku ya kiama, na hapo basi hapajahalalishwa mauaji humo kwa yeyote kabla yangu na hapajahalalishwa kwangu mimi isipokuwa saa moja tuu la mchana nayo ni haramu kwa uharamu Mwenyezi Mungu hadi siku ya kiama haung’olewi mwiba wake wala hawawindwi viwandwa vyake (ndege na wanyama) wala haviokwoti vilivyoanguka isipokuwa kwa ajili ya kuvitangaza wala haingolewei miti yake)). Ameipokea Imamu Muslim katika sahihi zake.

Na atakayeazimia kuingia katika nafasi hii ya amani basi ni wajibu juu yake ajiandae ili aingie katika hali ya amani kamili hadi kwa nywele zake na kucha zake ni wajibu aziache baada yakuhirimia hadi atakapomaliza ibada yake.

Hivyo hujifunza muislamu wakati wa hija kuheshimu haki ya uhai kwa kila kiumbe hai kwa hali yoyote atakayekuwa daraja lake kwa kuzingatia uislamu ni dini ya amani basi  asimkwaze yeyote na wala asimdhulumu yeyote na asimfanyie ujeuri yeyote.

Basi mataifa yana mahitaji makubwa na mifano hii katika nyakati  zetu hizi bila ya kuwasha moto wa ugomvi wa kumwaga damu na uchokozi wa kinyama kwa namna ya ugomvi mwingi wa wa nyama basi viumbe tunamahitaji makubwa ya kuingia katika amani ili kuondokana na umimi na mahakama na chuki na upasi na kiunukia pembe ya amani ya juu na tunajifunza maisha kwa amani kama anvyotaka Mwenyezi Mungu mtukufu kwa waja wake.

Ameema, kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu (Enyi watu sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke na tukakufanyieni mataifa na makabila ili mjuane kwa yakini mwenye ubora mbele ya Mwenyezi Mungu ni Yule mwenye kumuogopa sana Allah).

Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewaumba viumbe (Binadamu) analolitaka kwa viumbe wake ni kujuana na kuzoeana na wapendane wao kwa wao na wasaidiane kwa wema na kumcha Mungu na wema.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu (na saidianeni kwa wema na kumcha Mwenyezi Mungu na wala msisaidiane juu ya  madhambi na uadui.

Na anasema Mtume (SAW) msifanyiane uhasidi wala msilanguane wala msibughudiane wala msichunguzane na wala msiuze biashara mliyokuwa mnauza kwa mtu mwingine na muwe waja wa Mwenyezi Mungu mlio ndugu)) ameipokea Imam Muslim.

Na alikuwa kipenzi chetu Mtume (SAW) akiwalea masahaba  zake juu ya upendo na kilingania kheri na kukemea ubabe na kuwahimiza watu kwa anuani yake Mtume (SAW) amesema alikuwa Mtume (SAW) anapompa amri kiongozi katika Jeshi au uwakilishi humuusia katika mambo maalumu ya kumcha Mungu.

Na wale alionao miongoni mwa waislamu kwa kheri kisha husema ingieni vitani kwa jina la Mwenyezi Mungu, piganeni na wanaompinga Mwenyezi Mungu.

Piganeni na wala msipitukie mipaka, wala msifanye udanganyifu wala msiue watoto wala msitungike maiti kwani ni maneno haya ambayo anayasema Mtume (SAW) akiwausia viongozi wake huwakilisha mfano wa kimatengo wanalazimiana nao jeshi na wala hawatoki juu ya hilo kamwe hata kama kwa matatizo gani na hata kwa hali gani na hisotria ya ukombozi wa kiislamu inashuhudia kwa kiasi kikubwa na uchamungu wa jeshi la kiislamu.

MAKALA HII IMEANDALIWA NA

Sheikh Asayid Esmat

Mwalimu wa Az-hari Sharif

Tawi la Tanzania