KWA muda wa miongo kadhaa India na Marekani zimekuwa na mgogoro wa kuzozania mipaka hasa kwenye eneo la miinuko ya milima ya Himalaya ambayo inazitenganisha nchi hizo.

Mara kadhaa mataifa hayo makubwa yenye nguvu barani Asia, yamejaribu kutumia siasa kuutanzua mzozo huo, lakini inaonekana suluhu kamili ya mzozo huo iko mbali kupatikana.

Mnamo mwezi Juni 16 mwaka 2020, India ilithibitisha kuuawa kwa wanajeshi wake 20 baada ya kushambiliana na wanajeshi wa China waliokuwa wakilinda mpaka katoka bonde la Galwan.

Kilichofuata baada ya mashambulizi hayo nchi hizo zilionekana kuongeza wanajeshi kwa ajili ya mapambano zaidi na sio kutafuta suluhu ya mgogoro wa kuwania mipaka.

China imejitetea kwa kueleza kuwa bonde la Galwan ambalo lina ukumbwa wa kilomita skwea 38,000 ni la kwake na italilinda kwa gharama zote, huku India ikisema kuwa eneo hilo ni la kwake.

Katika kile kilichoonekana India inajiandaa kukabiliana na China, taifa hilo hivi karibuni limeingia mkataba wa kununua ndege tano za kivita aina ya Rafale, hali inayotafsiriwa kuwa inajiandaa kwa mapambano.

Jeshi la India limepokea ndege tano za kivita aina ya Rafale huku kukiwa na wasiwasi mkubwa kati yake na China.

Ndege hizo ni miongoni mwa makubaliano ya taifa hilo na lile la Ufaransa yaliofanyika mwaka 2016 kununua ndege 36.

Delhi inatumai kuimarisha jeshi lake la angani linalotumia ndege za zamani za kisoviet kupitia nununuzi dege hizo mpya.

Lakini watalaamu wanaonya kwamba ndege hizi haziwezi kutumika moja kwa moja iwapo kutakuwa na vita.

Mwanaanga mstaafu Pranab Barbora, ambaye alisimamia ununuzi wa ndege za kivita aina ya jaguar alisema kwamba kuwasili kwa Rafale ni hatua nzuri kwa sasabu itaimarisha uwezo wa jeshi la anga la India.