NEW DELHI, INDIA
WIZARA ya ulinzi ya India imetia saini kununua ndege 33 za kijeshi kutoka Urusi na 59 nyengine kuzifanya za kisasa zaidi zenye thamani ya dola bilioni 2.4, huku kukiwa na ongezeko la hali ya wasi wasi na nchi jirani ya China yenye silaha za kinyuklia.
Ununuzi wa ndege chapa MiG-29 na 12 SU-30 MKI, pamoja na ukarabati wa ndege nyengine 59 chapa MiG-29, ilikuwa kuweka sawa uwezo wa jeshi la anga la India.
Mifumo mipya na ya ziada ya makombora itakayotengenezwa nchini India pia ilinunuliwa kwa vitengo vyote vitatu vya jeshi la India.
Ongezeko la uwezo wa ulinzi nchini India lilichukuliwa kutokana na haja ya kuimarisha majeshi ya ulinzi ili kulinda mipaka ya nchi hiyo na wito wa waziri mkuu Narendra Modi wa India inayojitegemea.