ROMA,ITALIA

ULINZI  wa pwani ya Libya umesema meli ya kuwaokoa wahamiaji ya Ocean Viking imezuiliwa kutokana na hitilafu.

Shirika linaloendesha meli hiyo limetaja hatua hiyo ya Italia kama udhalilishaji.

Meli hiyo ilikuwa imekubaliwa kutia nanga katika bandari ya mji wa Sicily mnamo Julai 7 huku ikiwa na wahamiaji 180 ambao walihamishwa katika boti nyengine ili wakawekwe karantini kwa kipindi cha wiki mbili.

Wiki mbili hizo ziliisha siku ya Jumanne ingawa siku iliyofuata meli hiyo ilizuiliwa isiondoke.

Ulinzi wa pwani wa Italia ulisema baada ya kufanya uchunguzi walibaini kuwa ilikuwa na hitilafu za kimitambo.

Wahamiaji waliokuwa ndani wanatokea Bangladesh, Eritrea, Afrika Kaskazini na Pakistan na waliokolewa katika siku tofauti mnamo Juni 25 na 30.

Huku Ulaya ikiwa katika kipindi cha majira ya joto, jambo hilo huenda likawavutia wahamiaji wengi zaidi kuvuka bahari ya Mediterenia ambayo kwa sasa haina mawimbi.