ROMA,ITALIA

ITALIA  imeimarisha mazungumzo na Libya kuhusiana na ongezeko la idadi kubwa ya wahamiaji wanaowasili kutoka taifa hilo la Afrika Kaskazini wakitumia boti kwenye Bahari ya Mediterania.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia Luciana Lamorgese alifanya mikutano na Waziri Mkuu wa Libya Fayez Serraj na mawaziri wengine wa serikali yake mjini Tripoli.

Wizara hiyo ilisema  Lamorgese alisisitiza haja ya kuwahamisha watu kutoka vituo vya wakimbizi katika nchi hiyo iliyoharibiwa kwa vita, akisema mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaweza kusaidia katika kutimiza hilo.

Libya ni moja ya nchi kuu zinazotumiwa na wahamiaji wanaotafuta kuingia Ulaya kutokea Afrika.

Hali ya wakimbizi wanaotokea nje ya Libya katika makambi inazingatiwa kuwa hatari sana.