LONDON,UINGEREZA

WAZIRI  mkuu wa Uingereza Boris Johnson anajiandaa kufanyia mabadiliko makubwa sheria zinazohusiana na uhaini za taifa hilo.

Kwa mujibu wa Daily Mail iliyonukuu  kutoka ofisi ya waziri mkuu ya Downing Street, ilieleza kuwa mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa na Johson yatashuhudia sheria mpya ya uhaini, sheria mpya ya ujasusi kwa ajili ya kuwafuatilia mawakala wa nje na kuandikwa upya kwa sheria inayohusu siri za kitaifa ili iendane na enzi ya kidijitali.

Gazeti hilo limeyaelezea mabadiliko hayo kuwa ni makubwa kabisa yatakayogusa sheria zinazohusiana na uhaini tangu mwaka 1965 likisema yanafanyika ili kukabiliana na kitisho kinacholetwa na Urusi na China.