RAIS MAGUFULI atangaza siku saba za maombolezo ya kifo cha Marehemu Benjamin Mkapa,bendera kupepea nusu mlingoti kuanzia leo Ijumaa Julai 24, 2020.
Benjamin William Mkapa alikuwa rais wa awamu ya tatu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa ni rais wa kwanza kuchaguliwa kupitia mfumo wa vyama vingi vya siasa katika uchaguzi wa mwaka 1995. Mkapa alitanguliwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Ali Hassan Mwinyi, na aliongoza Tanzania kwa mihula miwili kuanzia 1995 hadi 2000 na 2000 hadi 2005.