LONDON , England
MSHAMBULIAJI, Harry Kane, amefikisha zaidi ya mabao 200 katika taaluma yake ya soka kwenye ngazi ya klabu baada ya kucheka na nyavu mara moja na kusaidia Tottenham kuilaza Newcastle katika Ligi Kuu ya Uingereza juzi.

Matokeo hayo yaliweka hai matumaini ya Tottenham ya kushiriki Ligi ya Europa msimu ujao wa 2020-21.

Hiyo ni baada ya kikosi cha kocha Jose Mourinho kufikisha pointi 55 kwenye msimamo wa EPL.
Nahodha huyo wa Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza, alipachika wavuni bao lake la 201 mwishoni mwa kipindi cha pili baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Martin Dubravka kutokana na shuti la Erik Lamela.(AFP).