NAIROBI,KENYA
KENYA imepokea timu ya madaktari 20 maalum kutoka nchini Cuba kusaidia nchi hiyo kukabiliana na janga la Covid-19.
Timu hiyo,iliyowasili jijini Nairobi jana, ni kutoka chuo cha Henry Reeve Medical Brigade kilichoundwa na Fidel Castro mnamo 2005 kushughulikia dharura na magonjwa hatari.
Balozi wa Kenya nchini Cuba,Anthony Muchiri, alisema kwa sasa timu hiyo iko Kenya.
“Ujumbe huo ni msaada ,isipokuwa gharama za usafirishaji na malazi, kwa kawaida hugharamia nchi inayopokea, ambapo ni miongoni mwa hatua tulionayo ya uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili,” alisema.
Cuba ilikuwa ikituma timu ya madaktari kwa nchi mbali mbali kama sehemu ya diplomasia yake ya matibabu.
Pia Cuba ilituma dawa kwa nchi mbali mbali za Ulaya kuwasaidia kukabiliana na idadi kubwa ya waathiriwa wa ugonjwa wa corona.