NAIROBI,KENYA

KENYA imerikodi kesi mpya ambazo ziliongezeka kwa masaa 24 yaliyopita na kuthibitishwa Waziri wa afya Mutahi Kagwe.

Idadi hiyo ilipatikana ndani ya sampuli 4, 522 ambazo zilifanyiwa uchunguzi katika masaa 24 ikiwa kwa sasa kuna sampuli 238,163 ambazo zinasubiri kufanyiwa uchunguzi .

Katika kesi hizo 425 ni za kiume wakati 263 ni za kike huku ambapo hali inaonesha kuwa mwanaume ndio wanaoongoza kwa idadi kubwa ya maambukizo nchini humo akiwemo mtoto mchanga wa miezi saba.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Embu, Waziri Kagwe alisema watu 457 walipona,401 wanahudumiwa nyumbani wakati 56 walitolewa hospitali na kurudi nyumbani.