INAELEZWA kuwa nafasi ya Kocha Mkuu wa Barcelona, Quique Setien ipo mashakani baada ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Celta Vigo, kwenye mchezo wa La Liga uliochezwa Jumamosi licha ya timu yake kuwa ya kwanza kutupia.

Mabao yote ya Barcelona yalifungwa na mshambuliaji wao Luiz Suarez dakika ya 20 na 67 ambaye alitolewa timu yake ikiwa imefungwa bao moja na Flyodor Smolov dakika ya 50 baadaye nafasi yake ikichukuliwa na Antoine Griezmann na ikafungwa bao la pili dakika ya 88 na Iago Aspas dk ya 88.

Ripoti zinaeleza kuwa wachezaji walimlaumu kocha kwa kushindwa kuwa na mpango mzuri wa mechi, jambo lililowafanya washindwe kulinda mabao yaliyofungwa na Suarez ambaye alikuwa kwenye ubora wake na nafasi yake kuchukuliwa na Griezmann.

Inaelezwa kuwa sio mara ya kwanza kwa wachezaji wa Barcelona kulalamika kuhusu kutoelewa mipango ya Setien kuhusu maamuzi ya kiufundi ambayo anaifanya akiwa kwenye mechi ngumu za ushindani jambo lililowapa nafasi Real Madrid kuwa vinara ndani ya La Liga yenye pointi 71 huku Barcelona ikiwa na pointi 69 zote zimecheza mechi 32