LONDON, England
MENEJA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema, anahitaji ubora zaidi kwenye kikosi chake ili kufikia lengo la kufuzu kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Lampard ameyasema hayo baada ya kukishuhudia kikosi chake kikifanya vizuri juzi usiku kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England kwa kuitandika Norwich City goli 1-0.
Mshambuliaji, Olivier Giroud ndiye aliyeipa matokeo mazuri Chelsea kwa kufunga bao la kichwa akimalizia krosi ya nahodha wa Marekani Christian Pulisic, mpira uliomshinda mlinda mlango wa Norwich, Tim Krul. (BBC Sports).