TRIPOLI, LIBYA

SHIRIKA  la kitaifa la mafuta nchini Libya (NOC), limeushutumu Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kwa kuamuru kurejesha tena marufuku dhidi ya usafirishaji mafuta, baada ya shehena ya kwanza ya mafuta kuruhusiwa ndani ya miezi sita iliyopita.

Umoja wa Falme za Kiarabu, Urusi pamoja na Misri zinaunga mkono Jeshi linalongozwa na mbabe wa kivita Khalifa Haftar (LNA) lililoko mashariki mwa nchi hiyo.

LNA ilisema, marufuku itaendelea hadi pale orodha ya matakwa yao itakapotimizwa, ikiwa ni pamoja na kuelekeza mapato yote ya mafuta kwenye akaunti mpya ya benki iliyoko nje ya nchi, kisha kugawiwa majimbo.

Hata hivyo hakukuwa na kauli ya moja kwa moja kuhusu shutuma hizo, kutoka UAE au kutoka LNA .