WASHINGTON,MAREKANI

MAAMBUKIZI  ya virusi vya corona duniani yameongezeka kupindukia watu milioni 15 jana, kwa mujibu wa idadi iliyowekwa pamoja na shirika la habari la Reuters.

Wakati ugonjwa huo ukishika kasi nchi bado zinaendelea kutofautiana katika jibu lao dhidi ya janga hilo.

Nchini Marekani, nchi ambayo ina idadi kubwa ya maambukizi duniani ikiwa na watu milioni 3.91 ya walioambukizwa, rais Donald Trump alionya, kuwa huenda hali itakuwa mbaya zaidi kabla ya kutengemaa.

Nchi tano za juu ambazo zina maambukizi makubwa ni pamoja na Brazil, India, Urusi na Afrika kusini.

Idadi iliyowekwa pamoja na shirika la habari la Reuters inaonesha ugonjwa huo unasambaa kwa kasi katika mataifa ya Marekani, ambayo yana zaidi ya nusu ya maambukizi duniani kote na nusu ya vifo.

Duniani kote pia kiwango cha maambukizi hakioneshi ishara ya kupungua kasi.