NA MWANDISHI WETU

LIGI Kuu Tanzania Bara jana imefunga pazia lake la mwisho kwa timu 10 kushuka uwanjani kusaka ushindi na baada ya dakika 90 kukamilika.

Vita kubwa ilikuwa ni kwenye timu zinazosaka nafasi ya kubaki ndani ya ligi, kucheza ‘playoff’ pamoja na zile zitakazoungana na Singida United kushuka daraja.

Baada ya dakika 90 kukamilika pointi zimewahukumu wakali watatu ndani ya ligi ambao maisha yao kwa msimu ujao yatakuwa ni ndani ya Ligi Daraja la Kwanza huku wawili wakisaka nafasi kupitia ‘play off’.

Wakali hao watatu wanaungana na Singida United na kufanya jumla ziwe timu nne ambazo zinashuka jumla daraja.

Alliance FC iliyo nafasi ya 17 kwenye msimamo ikiwa na pointi 45, Lipuli FC iliyo nafasi ya 18 na pointi 44, Ndanda iliyo nafasi ya 19 na pointi 41 pamoja na Singida United united iliyo nafasi ya 20 na pointi 18.

Zitakazocheza ‘play off’ ili kusaka nafasi ya kubaki ndani ya ligi ni Mbao FC iliyo nafasi 15 na pointi 45 na Mbeya City iliyo nafasi ya 16 na pointi 45.