YERUSALEMU,ISRAEL

MAELFU  ya raia wa Israel wameandamana wakipinga ukosefu wa ajira, ufisadi pamoja na namna waziri mkuu wa taifa hilo Benjamin Netanyahu anavyoushughulikia mzozo wa virusi va corona.

Polisi waliruhusu maandamano hayo nje ya makaazi binafsi ya Netanyahu yaliyopo katika mji wa pwani wa Caesaria,karibu na makaazi yake ya kiofisi mjini Jerusalem.

Netanyahu anakabiliwa na kesi ya ufisadi iliyofunguliwa mwezi Mei muda mfupi baada ya kuapishwa kuongoza serikali ya mseto pamoja na mpinzani wake waziri wa ulinzi Benny Gantz.

Waziri huyo mkuu mnamo mwezi Machi alisimamisha shughuli zote nchini humo ili kukabiliana na janga la corona lakini tangu alipotangaza kuviondoa vizuwizi hivyo mwezi Mei kumekuwa kukiripotiwa visa vipya kila siku hatua iliyoibua maandamano yaliyodumu kwa wiki nzima sasa na kuzidi kusambaa.