ISTANBUL, UTURUKI

MAELFU ya waturuki wamehudhuria sala za kwanza ya Ijumaa katika msikiti wa Hagia Sophia baada ya msikiti huo hapo awali kuwa kanisa.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alijiunga na waislamu wengine katika sala hio ndani ya msikiti huo wa Hagia Sophia ambapo pia mamia ya watu kadhaa walialikwa katika ibada hiyo.

“Waislamu wengi wameshiriki katika sala hii huku ukionekana kufurika hadi nje na wengine kukosa nafasi”, ilisema taarifa kutoka mjini Istanbul.

Mnamo Julai 10, Baraza la kiislamu la Uturuki lilikuwa limeidhinisha kubadilishwa kwa hadhi ya kihistoria ya Hagia Sophia kutoka kwenye jumba la makumbusho na kuwa msikiti, na kusababisha ukosoaji mkali kutoka nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ugiriki na Marekani

Mnara wa kumbukumbu ya miaka 1,500, ambayo ilitumika kama kanisa kuu na baadaye msikiti wa kifalme wa Ottoman, iliidhinisha tena jumba hilo la kumbukumbu la mwaka 1935, mwaka mmoja baada ya Mustafa Kemal Ataturk, mwanzilishi wa Jamhuri ya Uturuki, kupitisha mabadiliko yake na kuwa msikiti.