KIEV,UKRAINE

OFISI  ya rais wa Ukraine imesema maofisa wa nchi yake, Urusi pamoja na wa Shirika la Usalama na Ushirikiano Ulaya OSCE wamefikia makubaliano ya kusitishwa mapigano kati ya vikosi vya serikali na wanaotaka kujitenga.

Makubaliano hayo pia yalifikiwa na  wanaoiunga mkono Urusi huko mashariki mwa Ukraine.

Tangu mwaka 2014 makabiliano kati ya wanajeshi wa Ukraine na waasi hao wanaoungwa mkono na Urusi yalipelekea watu 13,000 kufariki dunia.

Volodymyr Zelenskiy

Vita vya kijeshi vilikwisha baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mwaka 2015 katika mji wa Minsk ila machafuko ya hapa na pale bado hushuhudiwa mara kwa mara na kusababisha vifo.

Katika taarifa yake Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alisema makubaliano hayo ni kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na ujumbe wa Ukraine wakiungwa mkono na Ujerumani na Ufaransa.