LONDON, England
MANCHESTER United inayonolewa na Ole Gunnar Solkjaer ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya yoso wa Manchester City, Charlie McNeill.

Nyota huyo raia wa England anayekipiga timu ya vijana ya taifa anatajwa kuondoka ManCity msimu ujao ambapo amedumu kwa miaka sita kwenye kituo cha kukuzia vipaji hapo Etihad.

McNeill kupitia ukurasa wake wa Instagram alishukuru kwa uungwaji mkono alioupata ndani ya miaka sita kwenye kikosi hicho huku akiwashukuru pia wachezaji wenzake pamoja na benchi la ufundi.

ManCity wameonekana kukubali kumruhusu kinda huyo mwenye miaka 17 aweze kuondoka huku ikielezwa kuwa wapo kwenye mazungumzo ya makubaliano na United.
Timu nyengine ambazo zimeonyesha nia ya kupata saini ya mshambuliaji huyo ni pamoja na Wolves pamoja na Leeds United.(Mail).