Wasifia uwepo wa maonesho hayo, Wasema yamekuwa na tija kwao

NA KHAMISUU ABDALLAH
TAMASHA la 44 la kimataifa la biashara maarufu kwa jina la sabasaba limemalizika hivi karibuni katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar- es Salaam huku likiendelea kuacha sifa nyingi zenye mafanikio kwa washiriki na wananchi waliotembelea kwenye mabanda mbalimbali.
Washiriki katika tamasha hilo wakiwemo wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo walilisifia na kuona umuhimu ulivyowatangaza kimataifa hasa kwa bidhaa zao mbali mbali hivyo kutoa fursa ya kujuana kati yao.
Mbali na wajasiriamali pia tasisi mbalimbali za serikali kutoka Tanzania bara na Zanzibar zilipata fursa ya kushiriki tamasha hilo huku wengi wao wakisema ni moja ya kudumisha Muungano uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Mbali na kujitangaza pia washiriki waliieleza makala hii kwamba tamasha la 44 la biashara kwao lilikua jukwaa lililowaongezea ujuzi na uweledi wa kujifunza mbinu kadhaa za uchumi na biashara, kubadilishana uzoefu wa kiuchumi na kukuza miaya ya biashara zao kati yao na taasisi mbalimbali za umma na binafsi.
Moja ya taasisi iliyopata mwamko mkubwa katika tamasha hilo la biashara ni Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) ambapo ushiriki wake ni mara ya pili kwenye maonesho hayo yaliyoanzishwa mwaka 1976 ambayo ilipata fursa ya kuelimisha watanzania utofauti wa ukusanyaji wa mapato kati ya bodi hiyo na TRA.
Wengi wa washiriki waliofika katika banda hilo walikuwa wakiiuliza maswali juu ya utozwaji wa kodi mara mbili ikiwemo ZRB na TRA.
Akizungumza na mwandishi wa makala haya, Ofisa Uhusiano wa Bodi hiyo, Badria Attai Masoud, anasema ushiriki wa maonesho hayo umewapa fursa ya kujitangaza zaidi.
Anasema tokea kuanza kwa maonesho hayo zaidi ya wananchi 500 wametembelea banda hilo na kupata elimu juu ya kazi zinazofanywa na bodi hiyo. 
Akielezea sababu ya ZRB kuamua kushiriki maonesho hayo, anasema maonesho hayo yanahusisha pande mbili za Muungano na wapo wananchi wanaoishi Tanzania bara na kufanya biashara zao Zanzibar na wanaoishi Tanzania bara wanaofanya biashara Zanzibar