NAIROBI,KENYA

MAONESHO ya Chakula vya Afrika yamefunguliwa mjini Nairobi yakiwa na lengo la kuimarisha minyororo ya thamani ya chakula wakati janga la virusi vya Corona likienea kote duniani.

Waandaaji wa maonyesho hayo walisema, kutokana na zuio la usafiri lililotekelezwa katika nchi mbalimbali ili kudhibiti janga hilo, maonyesho hayo yatafanyika kupitia mtandao wa internet wa “Global Trade Week”.

Habari zinasema, maonyesho hayo ya siku tano yataonesha mwelekeo wa maendeleo ya chakula na kilimo na bidhaa na teknolojia mpya za kisasa zitakazosaidia makampuni kupata maendeleo katika miaka kumi ijayo.

Washiriki 150 kutoka nchi na sehemu mbalimbali ikiwemo China wameshiriki kwenye maonyesho hayo.