NA MWANDISHI WETU

JANA Wazanzibari walifanya mapokezi makubwa ya mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Kujitokeza kwa umati wa wazanzibari na wana CCM kwa kiasi kikubwa kumeonesha Imani ya wazanzibari kumpokea kiongozi huyo na kuonesha dhamira ya dhati ya kutaka kumsimamisha madarakani.

Kutokana na maelezo yake wakati akiwahutubia wafuasi wake, Dk Hussein, alionesha Imani ya dhati juu ya upendo wao jambo ambalo linampa nafasi kubwa ya ushindi kupitia chama chake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu.

Ili nchi yoyote iweze kupiga hatua ya kimaendeleo ni lazima kuziba mianya ya rushwa, ubadhirifu na kujali maslahi ya umma ni miongoni mwa mambo anayotarajiwa kuanza nayo.

Licha ya msingi mzuri atakaoachiwa na mtangulizi wake, lakini kuna Imani kuwa kama ataytekeleza kwa vitendo yale aliyoahidi ni wazi kuwa nchii itafika mbali na kuwa ni moja ya mfano wan chi za visiwa.

Kwa miaka mingi sana Zanzibar inahitaji maendeleo zaidi kuliko yalivyo sasa hivyo kumpata kiongozi kama huyo kutazidisha kuimarisha maendeleo zaidi.

Kwa kuwa wazanzibari wanahitaji kuwa na kiongozi bora hivyo kauli yake aliyoitoa jana inakisi dhamira ya dhati aliyoionesha.

Miongoni mwa mambo aliyoahidi wakati atakapokuwa anatekeleza mambo ya maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar, hatokuwa tayari kuona watu wanashindwa kuwajibika na kuzorotesha mipango hiyo.

Kwa kuwa alisema hana shaka na mapokezi aliyopata huku akiamini kuwa ni dalili za ushindi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.

Kama tunavyofahamu kuwa msingi wa nchi hii ni Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, hivyo ahadi yake ya kuyaendeleza, kuyaenzi na kudumisha Mapinduzi hayo kwa vitendo na muungano uliodumu kwa miaka mingi ni jambo linalompa sifa kubwa ya kuwa kiongozi.