WASHINGTON, MAREKANI

HUKU Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani inaendelea kuongezeka, lakini serikali ya Marekani imeanza rasmi mchakato wa kujitoa shirika la afya la dunia WHO, kitendo ambacho kimelaaniwa vikali na jumuiya ya kimataifa.

Pande mbalimbali zinaona WHO ina umuhimu mkubwa katika kupambana na janga la COVID-19 duniani, kitendo cha Marekani cha kuamua kujitoa kwenye shirika hilo ni uthibitisho wa kutekeleza sera ya upande mmoja, ambacho kitavunja juhudi zake za kukabiliana na janga hilo na pia kimeathiri vibaya ushirikiano wa kupambana na janga hilo duniani.

Mtaalamu wa masuala ya kimataifa wa Kenya,Cavince Adhere, alisema Marekani kutangaza kujitoa WHO kunavunja ushirikiano wa pande mbalimbali na ushirikiano wa kimataifa, na kumepuuza maslahi ya binadamu na kulifanya shirika hilo kuwa jukwaa la ushindani wa kisiasa, lakini Marekani haitashinda daima.

Profesa wa chuo kikuu cha Dar es Salaam cha Tanzania Humphrey Moshi anaona wakati wa kukabiliana na janga la COVID-19, kitendo cha Marekani kitaongeza hali ya jumuiya ya kimataifa kutoiamini Marekani .