NA ZAINAB ATUPAE

HATUA ya makundi ya mashindano ya Chuo Kikuu cha Al-Sumait yamefikia tamati kwa kupigwa mchezo mmoja kati ya BG&History dhidi ya Linguistics.

Katika mchezo huo timu ya BG&History walifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuichapa mabao  5-1 timu ya Linguistics mchezo ambao ulitimua vumbi katika uwanja Chuo hicho kilichpo Chukwani majira ya saa 10:00 jioni.

Mtanange huo uliokuwa waushindani mkubwa ambao kila mmoja akisaka pointi tatu ili kuweza kutinga katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

Mabao ya BG&History yalifungwa  dakika ya  saba  na Omar Idd,bao la pili liliongezwa na Bakar Haji Soldado na bao la tatu lilifungwa na Omar Idd dakika ya 32 ambayo yalidumu hadi  mwisho wa kipindi cha kwanza.

Kurudi tena katika kipindi cha pili kumalizia mchezo huo timu hizo zilionekana kurudi uwanjani zikiwa na kasi kubwa,huku BG&History ikisaka nafasi ya kuongeza mabao na Linguistics kurudisha mabao kwa wapinzani wao.

Lakini dakika ya 78 Masoud Sultan wa timu ya BG&History aliongeza bao la nne na bao la tano lilimaliziwa na Omar Idd dakika ya 88 na bao la kufutia machozi la timu ya Linguistics lilifungwa na Abdalla Ali dakika 86.

Timu ambazo zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ni pamoja na BG&History,Science 1,Science 2 na IDCS ambapo nusu fainali ya kwanza itachezwa baina ya timu ya Science 2 na IDCS ambapo itatimua vumbi leo na fainali ya pili itazikutanisha timu ya Science 2 na timu ya BG&History.